
Shirikisho la soka duniani FIFA limeanzisha harakati za kumuadhibu
Mshambuliaji matata wa timu ya soka ya Uruguay Luis Suarez anakabiliwa
na marufuku ya mda mrefu itakayomlazimu kukosa mechi nyengine za
michuano ya kombe la dunia iwapo atapatikana na hatia ya kumng'ata
mchezaji wa Italy Giorgio Chiellini.
mcheza huyo kufuatia ushindi wa moja kwa bila dhidi ya Italy siku ya
Jumanne.
Jumanne.
Chiellini amedai kwamba Suarez alimng'ata bega lake licha ya Suarez kudai kuwa ni mchazaji huyo aliyemchezea vibaya.
Suarez mwenye umri wa miaka 27 huenda akapigwa marufuku ya kutoshiriki katika mechi 24 ama miaka miwili.

Refa aliyesimamia mechi hiyo kutoka Mexico Marco
Rodriguez hakuchukua hatua yoyote kufuatia kisa hicho,lakini FIFA bado
inaweza kumuadhibu Suarez.
Aliyekuwa mchezaji wa kiungo cha kati wa timu ya
Liverpool Jan Molby anatarajia kwamba Suarez atapigwa marufuku kwa
mechi zote za kombe hilo zilizosalia.
Raia huyo wa Denmark ameliambia gazeti la
Liverpool la Echo kwamba '' nina hakika FIFA itachukua swala hilo la
Suarez kama mfano kwa wengine''.
''Ni dhahiri kwamba matumaini yake ya kushiriki
katika michuano ya kombe la dunia iliosalia yamekwisha na ninataraji
kwamba FIFA itampatia marufuku ya mda mrefu''.



0 comments:
Post a Comment